Uhuru wa Kenya - Historia ya Kenya in Google

Uhuru wa Kenya Miaka kumi na tano ya Uhuru wa Kenya, kama ilivyokua miaka iliyopelekea uhuru, ilitawaliwa na sifa zilizomhusu Jomo Kenyatta miongoni mwa watu. Utawala wa Kenyatta uliofikia kikoma mnamo Agosti 1978, wakati kitabu hiki hakijakamilika, unaelezewa kwa ufasaha na. Kinaelezea mchango aliokuwanao Rais huyo katika muelekeo wa Kibepari (capitalist) na kijamaa (socialist) unaodhihirika katika mikakati ya kiuchumi nchini Kenya hivi sasa. Ushawishi wa ari ya “kinyakuzi” enzi za Kenyatta ulikuwa na athari zake. Jomo Kenyatta,

Historia ya Kenya inahusu eneo la Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Kenya. Historia ya Kenya kama nchi inayokaliwa na binadamu, inaenea miaka laki kama si milioni kadhaa. Kumbe historia yake kama nchi huru ni fupi. Uvumbuzi wa majuzi karibu na Ziwa Turkana unaonyesha kwamba kiumbe kama Australopithecus anamensis aliishi katika eneo ambalo sasa ni Kenya kuanzia miaka milioni 4.1 iliyopita. Lakini mabaki yaliyopatikana katika mabonde ya Tugen, yaliyokuwa na takriban miaka milioni 6, yalipelekea kutajwa kwa aina mpya ya spishi, Orrorin tugenensis.

Bendera ya Kenya (English:Flag of Kenya) ilizinduliwa rasmi tarehe kumi na mbili Desemba, mwaka wa 1963. Bendera ya Kenya ina msingi katika bendera ya muungano wa kitaifa wa Kenya African . Rangi zinaashiria weusi wengi wenyeji , nyekundu ni damu iliyomwagwa wakati wa mapambano ya uhuru, na kijani kibichi ni mali asili; mikanda meupe yaliongezwa baadaye na yanasimamia amani. Ngao nyeusi, nyekundu, na nyeupe ya jadi ya Kimaasai na mikuki miwili yanaashiria ulinzi wa mambo yote yaliyotajwa hapo juu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...