
Baada ya majadiliano na serikali ya Ukoloni ya Britain mnamo 1963, Serikali iliruhusu mfumo wa ‘’Kura moja kwa kila mmoja’’ mnamo 1963. Uchaguzi wa kwanza uliisha taratibu huku Jomo Kenyatta akichaguliwa kama Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya mnamo 1963. Mwaka uliofuata, chama chake cha KANU ilihariri katiba ya Kenya kumfanya Kenyatta Rais wa kwanza wa Kenya Chini ya uongozi wake, ushindani uliisha pole pole wakati vyama vya kisiasa vyote viliungana na, au kudhulumiwa na chama tawala cha KANU. ). Hii ilipelekea kuundwa kwa mfumo wa chama kimoja nchini mnamo hata baada ya kifo cha Jomo Kenyatta mnamo 1978. Kenya iligeuzwa rasmi kuwa nchi ya chama kimoja cha Kisiasa mnamo 1982 kufuatia mabadiliko ya katiba.
Baada ya maandamano ya Saba Saba mnamo 1990, KANU ilijikunja na kuanza mikakati ya kurekebisha mfumo wa kisiasa. Mnamo 1992, kipengele ambacho kilikuwa kimeifanya Kenya kuwa na mfumo wa Chama Kimoja kilifutwa na Kenya ikarejea kuwa na Mfumo wa Vyama Vingi.[1]. Uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo ulifanyika mnamo 1992 huku wa pili ukifanyika mnamo 1997. Katiba ya Kenya haikuwa imerekebishwa kutosha ili kuendeha mfumo huu. Hata hivyo, mnamo 2002, shughuli za uchaguzi zilitajwa kuwa za haki na huru na Jamii ya Kimaataifa, huku KANU ilkipokeza mamlaka kwa chama cha National Rainbow Coalition (NARC). Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari.